Mwaka 2017 East Africa Television LTD ilianzisha kampeni ya kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji shuleni.
Kampeni hii ilikuja baada ya tafiti kuonesha kuwa wasichana wengi hupata changamoto katika siku zao za hedhi kwa kushindwa kununua taulo za kike hivyo kupelekea kukosa masomo shuleni kwa takribani siku 3 mpaka 7 kwa mwezi za masomo.
2024 ni mwaka wa saba (8) tangu kuanzishwa kwa mradi huu, tukishiriana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) lengo kuu likiwa ni kuhakikisha watoto wa kike wanapata sio tu taulo za kike lakini pia wanakuwa na vyoo vizuri na maji safi mashuleni ili wabaki salama katika siku zao za hedhi.
Mwaka huu 2024, kampeni hii ina lengo la kufikia watoto wa kike 10,000 katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Lengo la Kampeni
Lengo letu kuu ni kumsaidia msichana huyu kwa kumpatia taulo salama na kuhakikisha hakosi tena masomo yake na anafikia ndoto zake.
'Unapomuinua mtoto mmoja wa kike, umeinua jamii nzima'
#Namthamini
#NasimamaNaye