Kituo cha East Africa Television Limited kimeandaa shindano kubwa la kucheza mziki lijulikalo kama Dance 100%. Shindano ambalo huwapa nafasi washiriki kutoka pande zote za Tanzania hasa wakiwa katika makundi.Ushiriki unakuwa katika hatua ya mchujo mara tatu na hatimae kufikia robo fainali, nusu fainali hadi kufika fainali.Shindano lote la Dance 100% pia inaonyeshwa katika luninga ya EATV.
Shindano la Dance 100% linaendeshwa na kampuni ya East Africa Television Ltd na kusimamiwa na Baraza la Sanaa Tanzania BASATA. Kusudi la mfululizo wa shindano hili ni kutambua vipaji vipya vya kucheza mziki kwa vijana ambao hawana fursa ya kuonyesha vipaji vyao.
Mashindano haya yalianza June 22, 2012 ambapo makundi 40 yalishiriki na kuongezeka mpaka kufikia makundi 62 mwaka uliofuata June 23, 2013. Shindano hilo linasimamiwa na jopo la majaji watatu ambalo hutoa majibu ya matokeo ya washindi.
Dance 100% limekuwa onyesho linalotajwa kuwa bora kwa vijana wa umri wa miaka (14–45) likuvutia makundi mengi ya ushiriki na idadi kubwa ya watazamaji kila mwaka.
Onyesho hili lina utaratibu ambapo huwapa nafasi washiriki kucheza mitindo tofauti ya mziki. Mashindano haya hufanyika maeneo tofauti jijini Dar es salaam na makundi yanayo shiriki huonyesha uwezo wao mkubwa wa vipaji na makundi yanayoshinda yanasonga mbele katika hatua nyingine ya robo fainali na kushindanishwa na makundi mengine ambayo yamepita na kufika hatua ya robo fainali.
Mwisho wa mchakato huo makundi kumi bora wanachaguliwa kwa ajili ya kushiriki katika hatua ya nusu fainali na hatimae fainali ambapo katika mchakato huo unakuwa na ushindani wa hali ya juu kwa washiriki.
Washindi wanapata fedha taslimu na kutangazwa kuwa washindi -"Mabingwa wa shindano la Dance 100% ". Katika misimu miwili iliyopita washindi walikuwa ni T-Africa mwaka 2012 na The Chocolate walikuwa washindi mwaka 2013.
Miaka miwili mfululizo (2013 na 2014) mashindano haya ya Dance 100% yamekuwa yakidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Na mwaka huu (2014) kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Grand Malt, ndio kimekuwa kinywaji rasmi cha mashindano ya Dance 100% (2014).
Shindano la mwaka huu lilianza Jumamosi ya tarehe, 19th Julai 2014, ambapo lilianza kwa usajili katika viwanja vya Don Bosco Upanga, ambapo mchujo wa pili wa usajii ulifanyika viwanja vya Don Bosco Oysterbay tarehe 26 Julai na usajili wa mwisho umefanyika viwanja vya TCC Temeke tarehe 3 Agosti 2014 na utafwatiwa na hatua ya robo fainali na kuendelea hadi fainali.