Katika kukuza vipaji na kurudisha heshima ya mpira wa kikapu Tanzania, mashindano ya Sprite BBall Kings yameanzishwa na Kituo cha East Africa Television (EATV) na East Africa Radio kwa ushirikiano wa kinywaji cha Sprite.
Mei 3, 2017 mashindano haya yalizinduliwa rasmi kwa jumla ya timu 52 toka pande mbalimbali Tanzania kujisajili.
Usahili wa timu, Hatua ya kufuzu , Timu 16 bora, Robo fainali, Nusu fainali na Fainali , ni hatua 6 muhimu zinazozingatiwa katika mashindano haya.
Ili kutia hamasa zaidi ya mashindano haya, zawadi mbali mbali ikiwemo fedha na tuzo maalum zinatolewa kwa washindi watakaofanikiwa kutwaa ubingwa kila mwaka.
"Together Tunawakilisha" ili kurudisha heshima ya mpira wa kikapu Tanzania.