Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Siku chache baada ya msanii mkali wa r&b bongo Belle 9 kuweka brich kichwa kizima mashabiki zake wamekuja juu kwa kumshushia matusi na maneno ya kumdhihaki kwenye mitandao.

Star wa Bongo Fleva Belle 9

Akizungumza na Enewz Belle alisema kuwa msanii yeyote ambae anaijua sana siku zote huwa hana mipaka na kazi yake anaweza akafanya kitu chochote kuhusiana na sanaa yake hivyo hata yeye hana mipaka kwani rangi hiyo aliyoiweka katika nywele ''brichi'' zake inamaana ya thamani ya mtu mweusi .

“Style tofauti tofauti za nywele mimi nilianza kuweka muda mrefu tangu sijaanza kufanya mziki mimi nilikuwa hadi nikisuka na hii rangi yangu ni nyeusi na kichwani nina gold nikiwa ninamaanisha watu weusi tunathamani maana nimekuwa nikiona watu weusi sehemu tofauti tofauti wakidharauliwa na kubaguliwa,

mimi nimependa vile kwasababu kuna watu katika mitandao ya kijamii wao kila kitu wanaona sawa na nashukuru kuona watu kwa mara ya kwanza wamepinga ambacho mimi nimefanya,mimi ninamashabiki wazuri kumbe nikifanya kitu wanaweza kunielimisha wapo huru na mimi hawanihofii yaani mashabiki zangu wapo wawazi kwangu”,alisema Belle 9.