Jumatatu , 19th Oct , 2015

Kamati ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, chini ya mwenyekiti Farough Baghoza imekutana hapo jana kwa ajili ya kupanga mikakati pamoja na kuunda kamati ndogondogo.

Baghoza amesema kamati hiyo imetoa nafasi kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa maoni yao kwa lengo la kuhamasisha na kuisaidia Taifa Stars kuitoa Algeria katika mchakato wa kuwania kucheza Kombe la dunia, Novemba mwaka huu.

Stars inawania kucheza Kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 na sasa itakutana na vigogo, Algeria ambao ndiyo timu bora Afrika kwa kipindi hiki ikiwa ni baada ya kuitoa Malawi.