Jumamosi , 26th Sep , 2020

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema unatarajia kupokea ripoti ya mwisho ya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa Klabu yao kutoka kwa wasimamizi wa zoezi hilo ambao ni Kampuni ya La liga mwanzoni wa mwezi wa kumi mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Yanga, Mhandisi Hersi Said.

Akizungumza na Kipenga, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mhandisi Hersi Said amesema bado wapo katika mchakato na pindi tuu watakapomaliza ndiyo wataenda kwenye uwekezaji wenyewe.

“Baada ya kutoka katika hatua ya kwanza ya mchakato wa mabadiliko ambao ni kupata huo utaalam kwa ndani, tutauleta huo utaalam katika matawi ya Yanga na kupata kile wanayanga watakachokishauri kutokana na ripoti hiyo na baadae tutaenda kwenye mkutano mkuu ili kupata baraka za wanayanga wote” Alisema Mhandisi Hersi