Mohamed Matumla kushoto katika moja ya mapambano yake.
Rais wa TPBC Chaurembo Palasa ameiambia Hotmix Michezo wameamua kuanza mwaka kwa kuweka mapambano mengi ili kukuza ngumi za kulipwa hapa nchini hasa kwa vijana na kimsingi maandalizi yote yamekamilika.
Hotmix michezo imefanikiwa kuzungumza na mabondia Mohamed Matumla Snake Jr na Mfaume Mfaume watakaopambana Februari 5 mwaka huu ikiwa ni moja kati ya mapambano hayo ambapo kila mmoja ametamba kumkalisha mwenzake siku hiyo.