Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Simba uso kwa uso na Al Ahly

Ijumaa , 8th Jan , 2021

Hatimaye wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Simba SC wamepangwa kundi A sambamba na mabingwa wa watetezi Al Ahly, Namungo nayo imepangwa kucheza na Primeiro De Agosto kwenye kombe la shirikisho hatua ya mtoano, kwenye droo iliyofanyiaka hii leo Cairo Misri.

Simba wamepangwa Kundi moja na Al Ahly , Al Merreik na AS Vita

Shirikisho la soka barani Afrika Caf, Alasiri ya leo imeendesha droo ya wazi ya upangaji makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika pamoja na kupanga timu zitakazokutana kwenye hatua ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

 

Wekundu wa msimbazi Simba ambaye ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika imepangwa kundi A na Al Ahly ya Misri, Al Merreik ya Sudan na AS Vita kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na michezo hiyo ikitazamiwa kuanza 14 Februari 2021.

 

Hii ni mara ya pili Simba kupangwa na Al Ahly ambayo ni bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo pamoja na klabu ya AS Vita ya DR Congo baada ya kupangwa nao kundi moja msimu wa mwaka 2018-19 msimu ambao Simba alifanikiwa kuishia hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika.

 

Simba walikata tiketi ya kucheza hatua ya makundi baada ya kuiondoa Plateua United ya Nigeria kwenye mchezo wa hatua ya awali kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0, kwenye hatua iliyopita ambayo ni raoundi ya kwanza wakaitupa nje ya mashindano FC Platnum ya Zimbabwe kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kwenye michezo ya mikondo miwili.

 

Klabu ya Namungo ambayo ndio wawakilishi wa Tanznaia kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikiwa inacheza mashindano haya kwa mara a kwanza imepangwa kucheza dhidi ya klabu ya Primeiro de Agosto ya Angola kwenye michezo miwili ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika, mchezo wa kawanza utachezwa kuanzia tarehe 14 februari 2021 na marudiano kupigwa tarehe 21 februari 2021.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali