Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Samatta aing'arisha Taifa Stars

Jumamosi , 25th Mar , 2017

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta leo ameing'arisha Taifa Stars kwa kuifungia mabao mawili na kuipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Mbwana Samatta (Kushoto) akimtoka mchezaji wa Botswana katika mchezo

Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa ulio katika kalenda ya FIFA, umepigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya watanzania wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi, akiambatana na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye.

Katika mchezo wa leo ambao umejumuisha kikosi kipya kabisa cha Taifa Stars, chini ya kocha mpya Salum Mayanga, kimeanza kwa kasi ya aina yake na kufanikiwa kupata bao la mapema kabisa kunako dakika ya 2 mchezo kupitia kwa nahodha Mbwana Samatta aliyeitendea haki pasi ya Mohamed Hussein.

Taifa Stars iliendelea kuonesha kandanda safi, licha ya ubora na uimara wa Botswana, lakini ikashindwa kutumia nafasi kadhaa ilizopata kupitia kwa Samatta, Ajibu na Msuva.

Kipindi cha pili kilianza kwa Botswana kuongea nguvu na kufanya mashambulizi mengi ambayo hata hivyo ukuta wa Taifa Stars uliokuwa ukiongozwa na Abdi Banda, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein na Shomary Kapombe uliweza kutulia na kuhimili.

Mabadiliko ya kuwatoa Shiza Kichuya, Frank Domayo, Ibrahim Ajibu na Himid Mao na nafasi zao kuchukuliwa na Farid Musa, Mzamiru Yasin, Salum Aboubakary na Jonas Mkude, yaliweza kuzaa matunda ambapo katika dakika ya 77 Mwana Samatta akaifungia Taifa Stars bao la pili kwa mpira wa adhabu alioupiga baada ya kuangushwa nje kidogo ya eneo la 18.

Hadi mwisho wa mchezo, Tanzania inaondoka na ushindi wa mabao 2-0, ushindi ambao una faida katika viwango wa vya ubora ambavyo hutolewa naFIFA kila mwezi.

Mara baada ya mchezo, Nahodha wa Botswana Lebogang Ditsele amelalamikia hali ya joto ambayo amesema kuwa imewafanya wakumbane na mchezo mgumu, lakini akasema ingawa si matokeo mazuri kwao, bado yana faida kwao kwa kuwa wapo katika hatua ya kujenga timu ambapo kikosi kilichocheza leo kwa kiasi kikubwa kimejumuisha wachezaji vijana ambao ni wageni katika kikosi hicho.

Kwa upande wa Mbwana Samatta, amesema jambo la muhimu leo ilikuwa ni ushindi kwa ajili ya kurejesha imani ya watanzania katika timu yao na pia kupanda katika viwango vya FIFA, ingawa wameonekana kutocheza kwa kasi ambayo ingewafurahisha zaidi watanzania huku akitoa pongezi kwa wachezaji wenzake kwa ushirikiano na kujituma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa na aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Nape Nnauye katika uwanja wa Taifa DSM wakishuhudia mchezo kati ya Taifa Stars na Botswana.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine