Jumanne , 27th Sep , 2016

Nahodha wa Simba Jonas Mkude amesifia safu ya ushambuliaji wa timu hiyo, kuwa ni moto mkali katika kuelekea mpambano wao na watani zao wa jadi Yanga, Jumamosi Oktoba 1 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washambualiaji wa Simba SC.

Safu hiyo ya Simba inaundwa na viberenge, Shiza Kichuya, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Jamal Mnyate, Yassin Mzamiru na Ibrahim Ajibu.

Mkude amesema wachezaji hao wana kasi kubwa na watasaidia kwa kiasi kikubwa Simba kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zijazo, na wamejiweka sawa kikosi kizima kulipiza kisasi cha kufungwa na Yanga katika mechi zote mbili za msimu uliopita.

“Soka ni mchezo wa makosa, unapofanya kosa ni lazima ujutie. Sisi tulifanya makosa wakayatumia vema, ndiyo maana nasema ni lazima tuwe makini kutorudia makosa kama yale ili kutimiza azma yetu,” alisema nahodha huyo.