Wachezaji wa Mbeya City
Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika asilimia mia moja,hasa baada ya program za mazoezi kufanyika kwa siku mbili kama ilivyokuwa imeelekezwa na kocha Kinnah Phiri na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za mchezo wa leo
"Tumekuwa na siku mbili nzuri za mazoezi tangu tulipofika hapa Shinyanga siku ya juzi, tumekamilisha maandalizi yote tunasubiri dakika 90 za kesho, tunafahamu Mwadui ni timu nzuri lakini matokeo huja kulingana na vile ambavyo umejiandaa, sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo ili kupata pointi tatu, lengo letu ni kuona tunakuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu". Amesema ten
Akiendelea zaidi Ten alisema nyota wote 20 walisafiri kwaa ajili ya michezo miwili ya kanda ya ziwa wako kwenye hali nzuri pasipo majeraha yoyote kwa mujibu wa taarifa ya daktari, na hakuna shaka kuwa wako tayari kuitetea timu yao kwa uhakika na nguvu zote.
Michezo mingine inayopigwa leo ni JKT Ruvu inayoikaribisha Mbao FC katika dimba la Mkwakwani Tanga, na African Lyon wanaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar.
Matokeo ya mechi za jana katika ligi hiyo yalikuwa kama ifuatavyo
Simba Vs Prisons, Feb. 11, 2017
Simba 3-0 TZ Prisons
Ruvu Shooting 0-0 Azam
Ndanda 0-0 Toto
Stand 0-0 Majimaji