Jumanne , 24th Jan , 2017

Rapa Madee ambaye hivi sasa amefanya vyema na wimbo wake 'Hela' amefunguka na kusema kuwa Rapa Nay wa Mitego amemsaidia sana kuipa nguvu kazi yake ya 'Hela' huku akimshauri kutumia muda wake kuzipa promo kazi zake.

Rapa Madee akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Jr Junior

 

Madee alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema Nay wa Mitego ameingilia kazi ya Babu Tale ya kuhakikisha ngoma hiyo inapata promo ya kutosha kila kona kutokana na vile anavyomzungumzia.

"Mimi namshukuru Nay wa Mitego kwani amepelekea kazi yangu kusikilizwa sana na kaipa nguvu maana sijatumia nguvu kubwa kuona ngoma inafanya vyema hivyo naweza kusema kwangu imekuwa faida, yaani ni kama ameingilia kazi ya Babu Tale kuona ngoma inapenya kila sehemu na kupata promo ya kutosha, ila namshauri siku nyingine ni bora ahangaikie kizipa promo kazi zake' alisema Madee 

Mbali na hili Madee alizungumzia wimbo wake huo wa 'Hela' na kusema kuwa alipanga na alikuwa ameongea na Fid Q ili aiandike verse ya pili lakini haikuwezekana kutokana na Fid Q kuwa busy hivyo aliamua kuikamilisha mwenyewe.

"Hela verse ya kwanza nimeandika mimi ila nilikuwa nasuasua, verse ya pili nilimpigia simu Fid Q apite pale Mj Record lakini alikuwa busy hakuweza kufika nikaona ngoja nimalizie mwenyewe" alisema Madee