Jumanne , 24th Jan , 2017

Aliyekuwa meneja wa lebo ya muziki wa bongo fleva ya Poz Kwa Poz (PKP) Mubenga amesema kwa miaka sita aliyokaa PKP haikumnufaisha chochote badala yake ilimpotezea muda wake na kumnufaisha mtu ambaye hakumthamini.

Mubenga

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Mubenga amesema yeye ndiye alikuwa "fundi" wa PKP na alikuwa akiwaongoza katika kila kitu kilichokuwa kinaendelea, japo baadhi ya mawazo yake hayakufanyiwa kazi na kila alichokuwa akikifanya PKP hakikuwa na malipo yeyote kwake.

Hata hivyo Mubenga hakusita kusema kwamba yeye ndiye aliitoa PKP ilipokuwa na kuifikisha pale ilipo lakini faida ya kile alichokifanya haikuonekana na mwisho wa siku aliamua kuondoka na kuanzisha kampuni yake.