Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Dkt. Mwakyembe aitumbua Miss Tanzania

Jumatatu , 25th Sep , 2017

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara yake imefuta mashindano ya Miss Tanzania kwa sababu yaligubikwa na ubabaishaji mwingi katika uendeshaji wake.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe ameeleza hayo baada ya kupita takribani miezi mitatu tokea alipokabidhiwa zawadi yake Miss Tanzania 2016/2017, Diana Edward ambayo ilizua maneno mengi katika mitandao ya kijamii wakidai zawadi hiyo ya gari waliyompatia Miss huyo ilikuwa imechakaa na kupewa nje ya wakati na kushusha hadhi ya mashindano hayo pamoja na kuvunja moyo kwa watu ambao walikuwa na lengo la kushiriki katika mashindano mengine yajayo.

"Mimi na wizara yangu tuna mikakati tofauti kabisa, tungependa vitu vyote tunavyo vianzisha viwe na muendelezo na siyo vianzishwe leo keshokutwa vimekatika. Niwatolee mfano kidogo tulikuwa na Miss Tanzania hapa chini lakini nimepiga marufuku kwa sababu ya uswahili mwingi ambao mimi siwezi kuukubali nikiwa kiongozi wa hii wizara, kwa hiyo nimewakatalia wote hakuna cha miss Tanzania", amesema Dkt. Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Dkt. Mwakyembe ameendelea kwa kusema "Endapo watataka kuendesha hayo mashindano nitahitaji zawadi ya mshindi wa kwanza kama ni gari iletwe ofisini kwangu niione na waniachie funguo yake pia zawadi ya mshindi wa pili hivyo hivyo ndipo nikaporuhusu. Maana kila mwaka zawadi ya mshindi wa kwanza imekuwa ikisumbua kutolewa kwa muhusika. Sasa huo mchezo hapana, hatuwezi kuona ukiendelea, ubabaishaji siyo kwa Tanzania ya leo"

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwakyembe amesema sasa anachokifanya ni kukaa chini na baadhi ya wadau wa masuala ya 'fashion' ili waweze kuyaboresha mashindano hayo yaweze kuwa bora na kufanyika kila mwaka bila ya kuwa na ubabaishaji.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine