Jumanne , 7th Jun , 2016

Msanii wa Bongo Fleva Baraka Da Price amefunguka juu ya kolabo zake anazofanya na wasanii mbalimbali wa nje ya Tanzania.

Msanii wa Bongo Fleva Baraka Da Price

Akizungumza na eNewz Baraka alisema kuwa anafurahishwa na kolabo hizo kwa kuwa zinampa marejesho kuwa kazi zake zinafanya vizuri si Tanzania tu bali hata Kenya na Uganda ndiomaana wasanii hao wanapokuja tu step ya kwanza wanamuhitaji yeye.

“Mara ya mwisho kaja King Kaka kafika anamtaka Baraka ,alikuja Jaguar kafika anamtaka Baraka, kaja Prezo step ya kwanza namtaka Baraka de Prince nifanyenae kazi na nimeshapata tena barua kutoka UG sitaki kumtaja ni msanii gani ila ni wasanii wawili wakubwa sana ambao ni kama kundi hivi wamekuja hapa wanataka kufanya kazi na mimi,” alisema Baraka.