Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Zitto atangaza kumpigia kura ya Urais Tundu Lissu

Ijumaa , 16th Oct , 2020

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema kuwa siku ya kupiga kura, atampigia kura mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu, kwa kuwa anamuamini sana na anayo dhamira ya dhati kwa wananchi.

Kushoto ni Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, na kulia ni mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 16, 2020, na Kiongozi huyo na kusema kuwa chama hicho kimeshauriana na kuona kuwa kuna haja ya kuchagua kiongozi ambaye atarejesha furaha na kuheshimu katiba ya nchi.

"Kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi nitapiga kura yangu kwa ndugu Tundu Lissu, huyu ndiye mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda mgombea wa chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo", amesema Lissu.

Aidha Zitto amewaomba Watanzania kwa pamoja wampigie kura Lissu na kusema kuwa, "Sisi ACT Wazalendo hatupo tayari kuwa kizuizi cha safari hii ya mabadiliko, nami kama kiongozi wa chama ninao wajibu wa kulieleza hilo kwa uwazi kwa niaba ya viongozi wenzangu wa kamati ya uongozi''.

Mbali na hayo Zitto amewataka Watanzania kuwachagua wagombea wa ACT Wazalendo katika majimbo na wagombea wa upinzani wenye nguvu zaidi, huku yeye akitoa msimamo wake thabiti juu ya mgombea gani atakayempigia kura.

Awali Chama cha ACT-Wazalendo kilimteua Benard Membe ambaye alipitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwania kinyang'anyiro cha urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya