Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Zahanati yapigiwa mfano wa kuigwa Tanzania

Jumatatu , 11th Apr , 2016

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,ameipongeza zahanati ya uturo wilayani Mbarali kuwa ni ya mfano Tanzania kwa kuzuia vifo vitokanavyo na mama wajawazito na watoto wachanga

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,

Waziri Ummy ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipoenda kutembelea zahanati hiyo na kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana katika kuzuia vifo hivyo.

"Ninawapongeza sana wananchi wote wa Uturo kwa kazi kubwa na nzuri katika kudhibiti vifo vya watoto wachanga na akina mama,nataka kuwathibitishia zahanati ya uturo ni ya mfano kitaifa.

Alisema haikubaliki kwa mwanamke yeyote Mjamzito kufariki kwa sababu ya kutimiza haki yake ya kuzaliwa ya kuzaa,wanawake wameumbwa kuzaa,hivyo hakuna mtu atakayeweka vikwazo mwanamke asizae

"Kila mwanamke anayebeba ujauzito, mategemeo yake yeye na kichanga watakuwa hai na salama,hakuna mwanamke anayebeba ujauzito kwa mategemeo ya mtoto wake kufariki"

Aidha,alisema anautambua mchango mkubwa kwa watoa huduma ngazi ya jamii kwa kufuatilia wanawake wote wajawazito kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito pamoja n jamii yote kuwajibika na kushiriki katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi

"Popote nitakapoenda na kusimama
kuzungumzia kupambana na vifo vitokanavyo na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,nitatolea mfano zahanati hii.

Hata hivyo waziri Ummy alisema Moja ya kipaumbele chake katika wizara hii nikupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga

Katika pongezi hizo waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto hakusita kuwapongeza wanaume wote kwa kuwa jeshi la kupambana na vifo hivyo"wanaume wote wa vitongoji vya ukwama,ukwishikiro,mtamba na ukwaviro asanteni sana ninyi ni wanaume bomba kwa kuwajali wenza wenu na watoto.

Awali mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Wilison Chotamganga alisema jitihada za kutokomeza vifo hivyo vilianza mwaka 1998 mara alipohamishiwa kijijini hapo na kukuta matuta (makaburi)madogo mengi hivyo akaamua kuunda uongozi wa watu watano kwa kila kitongoji na kuweka mikakati ya kuzuia akina mama kujifungulia nyumbani na kila mwanaume na mwenza wake wanahudhuria kliniki kuanzia ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa takwimu za tanzania zinaonesha kila saa moja mwanamke mmoja anafariki wakati wa kujifungua,hivyo kwa siku wanawake ishirini na nne wanafariki,720 kwa mwezi na takribani wanawake 8,600 wanafariki kwa mwaka.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine