Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waziri Mkuu ampa siku mbili Mkurugenzi

Jumamosi , 2nd Jan , 2021

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amempa siku mbili Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoni Ruvuma, Gaspar Balyomi, awe amepeleka gari katika shule ya Sekondari Tunduru kwa ajili ya kuwahudumia walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Ametoa agizo hilo leo Januari 2, 2021, wakati akikagua ukarabati wa shule ya sekondari Tunduru, baada ya mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate, kumueleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya usafiri.

"Mkurungezi Jumatatu lete gari moja hapa likiwa limeandikwa Shule ya Sekondari Tunduru, lije kutoa huduma kwa watoto na walimu wetu, hii shule ina wanafunzi zaidi ya 600 na walimu 28 lazima iwe na usafiri ambao hata mtoto akiugua afikishwe hospitali", amesisitiza Waziri Mkuu.

Kuhusu ukarabati uliofanyika shuleni hapo, Waziri Mkuu, ameridhishwa na ametumia fursa hiyo kumpomgeza mkuu wa shule, Mwalimu Amini Limia, pamoja na kamati ya ujenzi kwa kazi nzuri ya usimamizi waliyoifanya.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi wazingatie sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa shuleni hapo ili waweze kuishi vizuri. "Someni hasa sasa hivi ni wakati wa likizo mpo hapa mnaendelea na masomo hatutarajii mpate daraja la nne wala sifuri, kila mmoja ahakikishe anasoma na kupata daraja litakalomfikisha chuo kikuu"

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine