Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Tanesco haitapata faida kamwe"- Heche

Ijumaa , 25th Mei , 2018

Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA) John Heche amesema Shirika la Umeme nchini TANESCO halitaweza kupata faida mpaka kuisha kwa dunia kutokana na mkataba wa kifisadi waliongia na kampuni ya uzalishaji umeme ya Songas.

Heche amesema hayo leo Mei 25, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akichangia hoja mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati katika mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa kama mkataba huo utaendelea basi madeni ya TANESCO yatazidi kuongezeka maradufu.

“Mwenyekiti umesema hapa TANESCO wameanza kupata faida, kamwe mpaka dunia hii inaisha TANESCO hawatapata faida kwasababu mkataba walioingia na Songas ni mkataba wa kihuni na wizi ndiyo unasababisha shirika hili kuendelea kuwa na madeni na hata dunia hii inaisha kama mkataba na Songas utaendelea kuwepo madeni ya TANESCO yataendelea kuwa makubwa”, amesema Heche.

Mbunge huyo ameongeza kuwa kitendo cha TANESCO kuwa shirika pekee linalozalisha umeme nchini bila ya kuwa na mshindani imechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na mzigo wa kutoa huduma pamoja na madeni ambapo mpaka kufikia sasa TANESCO inadaiwa zaidi ya bilioni 900.

Bunge limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo jumla ya shilingi trilioni 1.69 imeizinishwa kwa matumizi ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine