Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa wakati mwingine ajali za kizembe zinatokea kwa waendesha bodaboda kutokana na kukimbia kutozwa faini kubwa kuliko wa uhalisia wa vyombo wanavyoviendesha.
"Lengo za faini hizo zitakua ni kwa ajili ya kutoa onyo kwa waendesha vyombo hivyo vya moto ambao takwimu zinaonyesha kwa sasa ndio wanasababisha ajali nyingi zaidi ambazo zinapelekea madhara kwa binadamu lakini pia wengi kuacha pikipiki vituo vya polisi kutokana na kushindwa kulipa faini hizo", amesema Mwigulu.
Msikilize hapa chini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akielezea zaidi.