Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali kuboresha huduma kwa watalii

Ijumaa , 24th Mar , 2023

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati mahsusi wa  kuwafanya watalii hao kuongeza siku  za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema hayo katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika leo katika ukumbi wa Utawala Annex Bungeni jijini Dodoma

Amesema moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za malazi kwa watalii kwa kuzirejesha hoteli za Wizara ambazo zinaendeshwa  na  Sekta Binafsi ambazo kwa ujumla wake  hazifanyi vizuri

Amefafanua kuwa na Serikali inaendelea  mikakati ya kuhakikisha hoteli hizo mara baada  kurejeshwa  zinakuwa kinara kwa kutoa huduma bora kwa watalii

Pia, amesema Serikali ina mkakati wa kuboresha maeneo ya fukwe na kuunganisha vifurushi vya safari za watalii
“Tuna mpango wa kuomba umiliki wa maeneo ya fukwe urudi Serikalini ambapo moja ya mikakati yetu kama Serikali ni  kuunganisha vifurushi vya Watalii  ili waweze kutembelea vivutio vingi zaidi katika safari zao kwa mfano wakitoka hifadhini, waende kutembelea maeneo ya malikale na wamalizie safari zao katika maeneo ya fukwe, hii itawafanya watalii waweze kuongeza siku za kukaa nchini na kuongeza mapato ya utalii” Mhe. Masanja amefafanua. 
Katika hatua nyingine, Mhe.Masanja amesema  Serikali inaendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na  kufanya utafiti wa kujua vivutio vipi vinapendwa zaidi.

“Moja ya mkakati wa Serikali ni kufanya utafiti wa vitu ambavyo watalii wanavipenda na pia kuvitangaza vivutio vya utalii na tumejifunza kwamba watalii wengi wanapenda kupumzika katika maeneo ya fukwe baada ya kutembelea maeneo ya hifadhi , malikale na mengineyo” Mhe. Masanja amesisitiza.

Kuhusu ukarabati wa barabara kwenye maeneo ya hifadhi Mhe. Masanja amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege hifadhini pamoja na kuweka mazingira wezeshi ili watalii wanapofika wafurahie huduma.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameishauri Serikali kuangalia namna bora ya kurahisisha mchakato wa uwekezaji wa mahoteli kwenye maeneo ya hifadhi ili kuboresha huduma za malazi kwa watalii.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Watendaji na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90