Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Polisi wafafanua ajali ya Zuchy

Jumamosi , 27th Apr , 2024

Jeshi la Polisi nchini limewataka watu wenye taarifa tofauti na si za uzushi/uwongo kuhusu ajali ya Mpiga picha wa mtandao wa MillardAyo na Ayo TV Noel Mwingila maarufu Zuchy wazifikishe kwa viongozi ili hatua zichukuliwe na sio taarifa za uzushi zinazosambaa mitandaoni

Polisi wamesema miongoni mwa taarifa za uzushi zinazosambaa mitandaoni ni zile zenye kichwa cha habari SHUHUDA ambazo zinaeleza kuwa "Zuchy kapata ajali na boda hit and run mbele ya mataa ya masana kama 100 mita hivi toka saa nane usiku dereva wa boda akapelekwa  hospital. Umoja wa bodaboda wamekaa na mwili barabarani pale wakiita Polisi kisingizio gari haina mafuta kweli. Pia taarifa hiyo inaeleza bodaboda walikaa na mwili hadi  wakafunga barabara ili kushinikiza Polisi waitwe."

Polisi wamesema usahihi wa tukio hilo ni kuwa  tukio hilo liliripotiwa saa kumi na dakika kumi na mbili alfajiri kuwa, kuna ajali imetokea eneo la Mbezi Makonde. Baada ya kupokelewa taarifa hiyo  Maafisa na Askari waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa Tamasha la Shangwe la Utawala lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers waliondoka wakiwa na gari ya Polisi  kuelekea eneo la tukio na kuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa taratibu zingine za kisheria.

Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa katika uchunguzi imebainika marehemu alipata ajali na pikipiki aliyokuwa amepanda yenye namba MC 436 CMU  iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye alipata majeraha na anaendelea na matibabu.

Hivyo, mara baada ya taarifa ya tukio hilo kutolewa na  kupokelewa, Maafisa na Askari Polisi  walifika kwenye tukio kwa wakati na kutekeleza yale yanayopaswa kutekelezwa kwenye eneo la ajali. Tunawashukuru bodaboda wa eneo hilo wanaojali utu wa binadamu kwa kuzuia magari yasimkanyage marehemu.
 

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali