Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kigwangalla aomba hawa wakamatwe

Jumanne , 26th Sep , 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwakamata watu wote waliohusika kuchakachua fedha za ujenzi wa jengo la Zahanati ya Neruma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara yake ya kuimalisha sekta ya afya wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo aliweza kukagua jengo  jengo la Zahanati ya Neruma,iliyopo Kata ya Neruma Wilayani Bunda, Mkoani Mara na kubaini milioni 29 fedha za ujenzi zikiwa zimechakachuliwa. 

Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isaack Mahela alimweleza Naibu Waziri kuwa, ujenzi wa jengo hilo umegharimu jumla ya milioni 29 kwa ajili ya kupanua na kuweka fremu za milango pamoja na madirisha, kitu ambacho kimeonekana hakiendani na uhalisia wa fedha hizo.

"Nakuagiza Mkurugenzi, uhakikishe unawasilisha nyaraka zote za fedha za jengo hili kwa TAKUKURU na wale wote waliohusika kupitisha fedha hizo na uwakabidhi TAKUKURU ili wafanye uchunguzi na kuchukua hatua zichukuliwe", amesema Dkt. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amesema kuwa taifa linataka kusonga mbele hivyo watu wanaokwamisha mchakato wa Rais wa kuwaletea maendeleo wananchi wake lazima wachukuliwe hatua ili watu wengine waogope kutafuna fedha za umma.

Jengo hilo ambalo pia limeonekana kuwa chini ya kiwango katika maeneo kuta zake, mchakato wa ujenzi wa jengo ulianza tokea  mwaka 2015 kwa nguvu za wananchi na baadae Halmashauri ilitenga fedha za kumalizia mchakato kiasi cha milioni 29, ambazo zimebainika kutafunwa na watendaji waliokuwa wanashughulikia zoezi hilo.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya