Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Katambi abainisha utekelezaji wa maagizo ya Rais

Jumatatu , 27th Jun , 2022

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi amebainisha utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati alipokutana na wenye Ulemavu Mnamo mwezi Machi, mwaka huu, Ikulu Chamwino Dodoma.

Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kupokea Changamoto zinazowakabili wenye ulemavu nchini na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.

Akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Wafanyakazi wenye Ulemavu tarehe 27 Juni, 2022 jijini Dodoma, Katambi amebainisha kuwa Rais Samia ametoa zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kukarabati vyuo vya Ufundi Stadi kwa wenye Ulemavu ambapo ukarabati huo unaendelea katika mkoa wa Tabora, Singida, Dar es salaam na Mtwara. 

Aidha, amefafanua kuwa vitajengwa vyuo vipya mkoani Kigoma na Mwanza, huku chuo cha Masiwani Tanga tayari kimeshafunguliwa.

Katambi ameomgeza kuwa tayari serikali imeiwezesha Hospitali ya KCMC ili iweze kuzalisha mafuta yanayosaidia kukinga mionzi ya jua kwa wenye ulemavu wa ngozi, lengo ikiwa ni uhamasishaji wa uzalishaji wa ndani wa mafuta hayo ili kuleta unafuu na uhakika wa upatikanji wake.

Aidha, Katambi ameeleza kuwa katika kuhakikisha haki inatendeka kwa Wenye Ulemavu, tayari Mhe. Rais Samia ametoa fedha kwa ajili ya kupitia Sera na Sheria zinazo wahusu Wenye Ulemavu, ikwemo; Waraka wa utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010, Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010.

Sera ya Huduma kwa Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu pamoja na Sera ya Taifa ya Vijana zinaendelea kufanyiwa mapitio.

Aidha, katika hatua nyingine Mhe. Katambi amesisitiza ujenzi wa majengo ya serikali kuhakikisha unazingatia miundo mbinu rafiki kwa wenye ulemavu. 
Hivyo amezitaka mamlaka za serikali na zisisizo za serikali kuhakikisha zinatekeleza Sera na Sheria za wenye Ulemavu nchini.

“Sera na Sheria yetu inasema 3% katika utoaji wa ajira kwa wenye ulemavu, tunaenda kufanya ukaguzi kwa  kuanza na mamlaka za serikali kuona ni namna gani zinatekeleza  pia tutaenda kukagua Sekta Binafsi. Tunazitaka Mamlaka, Asasi na Taasisi zisizo za serikali kutekeleza sheria za Wenye Ulemavu kama anavyotaka Mhe. Rais Samia”

Katambi ametaja hatua nyingine ambazo serikali inaendelea kutekeleza ni katika sekta ya elimu pamoja na Bima. Pia, suala la vifaa vya watu wenye Ulemavu jinsi ya kuangalia namna bora ya kuhakikisha vinapatikana kama serikali inavyotaka.

Katika hatua nyingine, Mkurungenzi wa Taasisi ya Ikupa Trust Fund ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Stella Ikupa, ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassann kwa kuyapa kipaumbele masuala yanayowahusu wenye Ulemavu nchini. Aidha, ameipongeza serikali kwa kuendelea kuajiri wenye Ulemavu.

Mkutano huo ulioandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya  Ikupa Trust Fund, Kaulimbiu yake ni; “Stahiki Bora, Haki ya kuajiliwa, na Mazingira rafiki ya kazi  kwa Watu Wenye Uleamavu”

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine