Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Haya ndiyo mafanikio ya serikali ya Magufuli

Jumamosi , 15th Aug , 2020

Msemaji Mkuu wa serikali Dkt Hassan Abbasi amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais Dkt John Pombe Magufuli imefanikiwa katika utekelezaji wa sera zake katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya, miundombinu na uboreshaji wa uwekezaji.

Msemaji Mkuu wa serikali Dkt Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani)

Dkt Abbasi ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitano ambapo miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa  uzalishaji wa umeme nchini kutoka megawati 1,308 mwaka 2015  hadi kufikia megawati 1,602.32 mwaka 2020.

Kwa upande wa mageuzi kwenye Sekta ya Madini amesema “Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa”.

Kwa upande mwingine ni uendelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia, mradi wenye lengo la  kusindika gesi asilia kuwa kimiminika. “jumla ya TZS Bilioni 5.2 imelipwa kwa wananchi 618 kati ya 693 watakaopisha mradi katika eneo la Likong’o, Lindi.”, amesema.

Akielezea mafanikio katika upatikanaji wa umeme wa uhakika, Dkt Abbasi amesema hadi kufikia Julai, 2020 jumla ya vijiji 9,412 vimeunganishwa kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015, ikiwa ni sawa na ongezeko la vijiji 7,394 huku akisisitiza uendelezwaji wa miradi mingine kwaajili ya kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Serikali ya awamu ya tano pia imetumia takribani TZS Trilioni 1.109 ya fedha za ndani kutekeleza miradi mikubwa miwili ya umeme wa gesi: Kinyerezi-I Extension megawati 185 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na zaidi ya TZS Bilioni 315.4”.

Dkt Abbasi hakusita kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini ambapo amesema katika mageuzi kwenye Sekta ya Madini. “Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa”.

Amefafanua zaidi na kusema kuwa moja ya mafanikio ya serikali ya wamu ya tano katika Sekta ya Madini hadi Juni, 2020 ni pamoja na kuongezeka kwa masoko ya  madini 31 na vituo vya ununuzi wa madini 39 vilianzishwa maeneo mbalimbali nchini.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya