Azan Zungu ameyasema hayo katika hafla ya 15 ya kuhitimu elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya wasichana ya Babro Johansson ya jijini Dar es salaam.
"Niwasihi hakuna sheria yoyote itakayofungwa na bunge itakayozuia mimba za utotoni, hakuna sheria iitakayozuia mimba mashuleni, mimba zitazuiwa na nyinyi pamoja na wazazi wenu na jamii kiujumla", amesema Azan Zungu.
Azan Zungu ameendelea kwa kuwataka wanafunzi wengine kujitunza ili kuweza kuhitimu elimu yao salama, na kuja kujikomboa hapo baadaye na kujenga taifa lenye wasomi.
Tazama video hapa chini