Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Benki Kuu Tanzania yakanusha kuhusu deni la Taifa

Jumamosi , 19th Mei , 2018

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefunguka na kuwataka wananchi wa Tanzania kuzipuuza taarifa zinazosambaa zinazohusu ongezeko la deni la Taifa na kusema takwimu hizo zilizotumika sio sahihi zina lengo la kupotosha umma.

BoT imetoa ufafanuzi leo Mei 19, 2018 kupitia Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki baada ya moja ya chombo cha habari nchini Tanzania kuchapisha habari zilizokuwa zikidai kwamba deni la Taifa liliongeza kwa shilingi trilioni 12 katika deni la taifa kati ya Disemba 2017 na Machi 2018, takwimu ambazo sio sahihi.

"Takwimu sahihi ni kwamba deni la serikali pekee liliongezeka kwa sh. trilioni 2 kutoka sh. trilioni 47 hadi sh. trilioni 49. Deni hilo linajumuisha mikopo kutoka nchi wahisani, mashirika ya fedha ya kimataifa pamoja na mabenki ya kibiashara ya kimataifa wakati deni la ndani la serikali linajumuisha dhamana za serikali za muda mfupi na hati fungani za serikali pamoja na madeni mengineyo", imesema taarifa hiyo.

Aidha, BoT imesema deni la nje la sekta binafsi kati ya mwezi Disemba 2017 na Machi 2018 liliongezeka kwa shilingi trilioni 1.0 tu, kutoka shilingi trilioni 9 hadi shilingi trilioni 10 ambapo deni la Taifa linajumuisha deni la serikali la ndani na nje na deni la nje la sekta binafasi ambalo liliongezeka kwa shilingi trilioni 3 kutoka shilingi 56 mwezi Disemba 2017 hadi shilingi trilioni 59 mwezi Machi 2018.

"Ongezeko la deni la Taifa linatokana na mikopo mipya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na malimbikizo ya riba, hasa kutoka nchi za kundi lisilo la wanachama wa Paris, ambazo hazijatoa misamaha ya madeni kulingana na makubaliano...  

Pamoja na ongezeko hilo, deni la Taifa bado ni himilivu. Kuongezeka kwa deni la Taifa kunatokana na jitihada za serikali kujenga mazingira bora zaidi ya kuongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali za uchumi ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025", imesisitiza taarifa hiyo.

Mbali na hilo, BoT imesema badala ya kulinganisha takwimu zinazofanana, chombo hicho kililinganisha takwimu za deni la serikali la Disemba 2017 na deni la Taifa la Machi, 2018 ambazo zinajumuisha vitu tofauti. 

Kwa upande mwingine, BoT imetoa wito kwa vyombo vya habari kuomba ufafanuzi wa masuala yanayohusu taasisi hiyo ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza kwa kuchapisha taarifa zisizo sahihi.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine