Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania ateta na TEF

Alhamisi , 23rd Mar , 2023

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe de Boer amekutana na viongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), katika ofisi za ubalozi huo, jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha utendaji kazi wa vyombo vya habari

 

Balozi Boer amesema Rais Samia  ameonesha mfano bora.

“Nampongeza rais kwa kufungua milango katika utendaji kazi wa vyombo vya habari Tanzania, vyombo vya habari sasa visiwe vioga katika kutekeleza majukumu yake.

“Rais ameoonesha namna anavyohitaji vyombo hivyo kuwa huru, wanahabari nao watumie nafasi hiyo kuimarisha uhuru wao,” amesema Balozi Boer.

Katika hatua nyingine Balozi Boer huyo amesema, Rais Samia amefanya jambo kubwa kwa kuunganisha umoja hasa kwa kushirikiana na vyama vya upinzani katika mambo mbalimbali.

“Jambo analofanya Rais Samia ni la kupongezwa, hatua ya kushiriki kwenye mikutano ya vyama vya upinzani, inaonesha kwa kiwango kikubwa anataka kuunganisha nchi.

“Hii ni fursa ya kujenga nchi moja na kushirikiana kujenga uchumi imara. Ni vizuri kwa sasa na vyombo vya habari visiogope kufanya kazi na vyama vya upinzani kwa kuwa hata rais kaonesha kwamba hakuna tatizo,” amesema.

Pia ameipongeza TEF na wadau wa habari kuonesha mshikamano katika kupigania uhuru wa habari na kwamba, jambo lolote huenda taratibu mpaka linafanikiwa.

Deodatus Balile, Mwenyekti wa TEF amempongeza Balozi Boer kwa nchi yake kuwa karibu na vyombo vya habari Tanzania.

Hata hivyo, amemhakikishia kwamba vyombo vya habari vya Tanzania vinatarajia kuwa na sheria inayokuza tasnia ya habari na si inayoweka vikwazo vinavyoweza kuua kabisa thamani ya tasnia hiyo.

“Tuna imani na mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari, rais na serikali yake alionesha mapema nia ya kuondoa vikwazo katika uhuru wa habari nchini kwetu. Ndio maana maana baada ya kuingia madarakani alianza kufungulia vyombo vilivyokuwa vimefungwa ambavyo ni MwanaHalisi, Mawio, Raia Mwema na Tanzania Daima pamoja na Televisheni za mtandaoni.

"lakini hata katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Habari, kuna vikwazo vimeondolewa ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maeleza kupunguziwa mamlaka,” amesema.

HABARI ZAIDI

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria