Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Vikwazo vya biashara vyaondolewa EAC

Jumamosi , 29th Mei , 2021

Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki lakubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara na kuimarisha biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Baadhi ya mawaziri wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano.

Awali akifungua mkutano Jijini Arusha, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani utawawezesha mawaziri kupitia na kujadili miongozo ambayo itasaidia kuboresha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara. 
 
Naibu huyo amewataka mawaziri wahakikishe kuwa  uzalishaji wa bidhaa zinazouuzika unakuwa mkubwa ili kuboresha ushindani wa kibiashara katika jumuiya ambao utasaidia kuboresha uwekezaji wa ndani na uwekezaji wa nje.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana mambo mengi ya msingi ikiwemo kuendelea kuondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kikodi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe amesema kuwa mawaziri wamekubaliana kutoa msukumo wa biashara katika jumuiya ya afrika mashariki izingatiwe na kupewa kipaumbele na kuruhusu sekta binafsi kufanya biashara katika nchi mbalimbali.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Kenya Mhe. Betty Maina, Waziri wa Viwanda na Biashara, - Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda - Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban na wengineo.

Mkutano huu ni maelekezo ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Kenya tarehe 04 hadi 05 Mei, 2021.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine