TIGO yaja na Smart Kitochi

Jumanne , 13th Oct , 2020

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua simu mpya aina ya Tecno smart Kitochi ambayo sasa itapatikana kwenye maduka yote ya Tigo.

Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Tigo Mkumbo Myonga, Kulia ni Meneja mawasiliano Tigo Woinde Shisaeli

Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja wa bidhaa za Internet wa Tigo Mkumbo Myonga, amesema simu hizo zenye ubora zimezingatia mahitaji ya wateja wa Tigo wakiwemo wa hali ya chini

“Simu hii ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji na mteja atakaenunua atapata huduma ya Facebook toka Tigo kwa mwaka mmoja bure” amesema Mkumbo

Amesema kwa sasa wateja wa Tigo wana fursa kubwa ya kutumia simu hiyo kutokana na bei yake kuwa ya kawaida