Tamasha la Swahili Fashion Week 2013 lilofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 8 hadi 10 Desemba 2013 katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wabunifu wa nguo mbalimbali toka Afrika, waliweza kuonyesha ubunifu wao na kwa siku hizo tatu na kufanya tamasha hili kuwa gumzo kwa hizo siku tatu zote ambazo tamasha lilikuwa likiendelea.
Pia wanamitindo chipukizi nao walipewa nafasi kuonyesha vipaji vyao kwa kubuni nguo na kuzionyesha katika maonyesho hayo, na sio Tanzania pekee ila kutoka sehemu mbalimbali za Afrika.
Kama ilivyo desturi, tuzo kwa watu mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya mitindo na ubunifu waliweza kupata tuzo zao ili kutoa hamasa ya kufanya vizuri zaidi katika fani hii.
Pia East Africa Radio/Television kwa mwaka 2013, waliendelea kutoa udhamini wao katika tamasha hili kubwa la mitindo hapa Afrika Mashariki.