Jumanne , 27th Sep , 2022

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa taarifa za Patrick Aussems aliyekuwa kocha wa timu hiyo pamoja na makocha wengine wanaotajwa itajulikana hivi karibuni uongozi utakapokamilisha mchakato wa kufanya tathmini.

Patrick Aussems

Simba kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu,Juma Mgunda ambaye amepewa mkataba wa muda na yupo na kikosi hicho Zanzibar kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kuna makocha wengi wanahitaji kufanya kazi na timu hiyo ila wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

“Iwe huyo ambaye unamtaja, (Aussems) ama hao wengine wanaotajwa hatuwezi kuweka wazi majina yao mpaka mchakato utakapokamilika kwani kwa sasa kikosi kinaendelea na mipango yake. Juma Mgunda ambaye yupo na timu uwezo wake unaoneana kwenye mechi tatu kashinda zote na tena ni mechi ngumu ukianza za kimataifa mbili pamoja na ligi dhidi ya Tanzania Prisons hii inamaanisha uwezo wake sio wa kubeza, mashabiki wawe na utulivu,” amesema Ally.