Yanga yatoa tamko kuhusu Haji Manara

Ijumaa , 19th Feb , 2021

Klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Fredrick Mwakalebela, imesema tayari imeshachukua hatua dhidi ya Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara kwa kitendo cha kuchafua Chapa yao.

Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo Februari 19, 2021, Mwakalebela amesema wametoa siku 14 kwa Manara kuhakikisha anaomba radhi hadharani.

''Kuna mtu anaitwa Haji Manara, amekuwa akidhihaki sana brand yetu mpaka ametuletea matatizo na mdhamini wetu, tumempa siku 14 ajitokeze hadharani kuomba radhi na tumemfikisha kwa TFF pia hatua zichukuliwe na iwe fundisho kwa wengine'', amesema Mwakalebela.

Aidha Mwakalebela ametoa ufafanuzi kuhusu suala la Bernard Morrison, ambapo ameitaka TFF kuchukua hatua.

''Suala la Morrison tumeshapeleka malalamiko yetu kwa TFF kuwa kuna mkataba feki tunaomba tuitwe kuthibitisha lakini hatujaitwa, ila la mtu wetu Hassan Bumbuli limefanyiwa kazi na akafungiwa, kiukweli tunashangaa'' amesema.