Jumanne , 20th Apr , 2021

Klabu ya Yanga imemtangaza Nasreddine Al Nabi raia wa Tunisia kuwa kocha wake mkuu baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kukiona kikosi hicho kuchukua mikoba ya Cedric Kaze aliyefutwa kazi Machi 7 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo mzunguko wa pili.

Kocha mpya wa Yanga, Nasreddine Al Nabi kutoka Tunisia (katikati) akionge mbele ya wanahabari leo.

Akizungumza na wanahabari Habari wakati wa utiaji saini kaimu mtendaji wa Yanga Haji Mfikirwa amesema kuwa imekuwa ni safari ndefu, tumepita na waalimu tofauti hiyo yote ni katika kujenga kikosi chetu na kuwa bora.     

“Leo tumeingia mkabata na mwalimu pamoja na kocha wake msaidizi na atakuja pia mwalimu wa fitness na tumeamua kuchukua utaratibu huu tumpe mwalimu nafasi ya kufanya kazi yake vizuri aje kufanya kazi na watu ambao alishafanya nao kazi  huko alikopita” amesema Haji Mfikiriwa.

Kwa upande wake kocha huyo mpya wa Yanga Nasreddine Nabil amesema “Ninaijua vizuri na nina amini kwamba nitafanya vizuri hivyo ninashukuru kwa nafasi ambayo nimeipata nitatoa ushirikiano na kufanya kazi kwa ufanisi”.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza jumla ya mechi 25 na kukusanya pointi 54, saa 1:00 usiku wa leo Aprili 20, 2021 itakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 kwenye msimamo na alama 30 na imecheza mechi 24.

Kocha huyo ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa miongoni mwa timu ambazo alifundisha ni pamoja na Al Merrikh ya Sudan ambayo iliishia hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya bili kufungana na Simba Sportsd Club kwenye hatua ya makundi, wakiwa wote kundi A.