Yanga SC yaishtumu TFF kuihujumu

Ijumaa , 19th Feb , 2021

Klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu wake Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela, imesema haitendewi haki na mamlaka za soka nchini.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela akiongea na Wanahabari mchana wa leo kuelezea malalamiko yao ya kuhujumiwa.

Mwakalebela ameyasema hayo leo Februari 19, 2020 kupitia mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema kutotendewa haki huko kunasababisha wakose matokeo mazuri kwenye ligi kuu soka Tanzania bara.

''Sisi Yanga hatutendewi haki na vyombo vinavyosimamia mpira, TFF, Bodi ya Ligi, Kamati ya Saa 72, Kamati ya Waamuzi na mamlaka nyingine za soka, ndio maana tumekuwa tukipoteza pointi kwenye mechi nyingi'', amesema Mwakalebela.

Aidha ameongeza kuwa, ''Tumenyimwa penati dhidi ya Mbeya City, dhidi ya Kagera Sugar na mwisho tunakuwa tunakosa pointi katika hali ya kuonewa mpaka tunajiuliza kuwa, je, kwa mazingira haya kuna bingwa ameandaliwa?''.

Pia ameeleza kuwa endapo wataendelea kutendewa hayo basi watafikiria kujitoa. ''Kwa haya tunayofanyiwa na mamlaka mpaka tunajiuliza kama kuna bingwa ameandaliwa basi sisi tuondolewe kwenye ligi basi apewe ubingwa wake''.