Jumanne , 30th Jan , 2024

Uongozi wa Yanga SC umebainisha utakuja kivingine mashindano ya kimataifa yanayosimamiwa na CAF pamoja na Ligi Kuu Bara ili kuwapa burudani wananchi pamoja na kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo watacheza.

‘’Katika kipindi hiki cha mapumziko tumekitumia vyema katika kuboresha kikosi chetu hivyo naamini mashabiki wa Yanga wasubiri kupata burudani kutoka ndani ya kikosi chao’’ amesema Kamwe.

Miamba ya soka nchini Dar Young Africans dhidi ya Hausing FC kunako dimba la Azam Complex Chamazi saa 1:00 jioni katika mashindano ya Kombe la FA.