Yanga kutangaza zabuni ujenzi wa uwanja

Jumapili , 13th Sep , 2020

Klabu ya soka ya Yanga imesema imekamilisha kazi ya michoro kwenye ujenzi wa uwanja wake wa Kigamboni jijini Dar es salaam.

Kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii imeeleza kuwa hatua inayofuata ni kutangaza zabuni ili kazi ya ujenzi ianze rasmi.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa ujenzi utafanyika kwa ushirikiano na wadhamini wa klabu hiyo pamoja na wana Yanga wote kwa ujumla.