Jumatatu , 25th Sep , 2017

Beki kisiki wa klabu bingwa ya Afrika Mashariki na kati Azam FC, Yakubu Mohammed ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti kutoka katika klabu yake Azam.

Beki kisiki wa klabu bingwa ya Afrika Mashariki na kati Azam FC, Yakubu Mohammed.

Hayo yamebainishwa na taarifa kutoka katika kurasa maalum ya timu hiyo na kusema Yakubu amekuwa mchezaji wa kwanza wa Azam FC kuitwaa tuzo hiyo ikiwa imeanzishwa msimu huu ikidhaminiwa na wadhamini wa timu yao.

Yakubu Mohammed amekabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika viunga vya Azam Complex ambapo ulichezeka mchezo wao dhidi ya Lipuli FC.