Kagera Sugar wameshinda mchezo 1, kwenye michezo 5 ya mwisho waliocheza dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo wa mapema unachezwa Saa 8:00, mkoani Shinyanga katika dimba la Mwadui Complex, ambapo Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Dodoma Jiji FC. Wenyeji Mwadui hawajashinda mchezo hata mmoja kwenye michezo yao 10 ya mwisho na ndio wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 12.
Dodoma Jiji wana alama 22 wapo nafasi ya 8 na wameshinda michezo 3 kwenye michezo 5 ya mwisho. Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya timu hizi ambao ulipigwa Jijini Dodoma ulimalizika kwa Dodoma Jiji kushinda kwa bao 1-0.
Saa 10:00 kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, JKT Tanzania watakuwa wanawaalika Kagera Sugar, timu hizi zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa zinatofautiana alama 5 kwenye msimamo wa ligi, Kagera Sugar wapo juu ya JKT Tanznaia wakiwa na alama 22 katika nafasi ya 7, wakati JKT wao wapo nafasi ya 15 na alama zao 17.
Mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, JKT Tanzania waliibuka na ushindi wa bao 1-0, na JKT wameifunnga Kagera kwenye michezo yote 4 ya mwisho waliokutana, na katika michezo 5 ya mwisho Kagera Sugar kashinda mara 1 tu.