Yanga na Mazembe zote zimefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa wapinzani wao juzi na jana.
Mazembe walianza kufuzu juzi kwa faida ya bao le ugenini, baada ya sare ya jumla ya 2-2 dhidi ya Stade Gabesien ya Tunisia ikishinda 1-0 nyumbani Lubumbashi wiki iliyopita kabla ya juzi kufungwa 2-1 Tunisia.
Yanga ikafuatia kufuzu jana kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola baada ya kufungwa 1-0 mjini Dundo ikitoka kushinda 2-0 wiki iliyopita Dar ea Salaam.
Ulimwengu ameipongeza sana Yanga kwa kufuzu mashindano hayo na kuongeza kuwa hayo ni matunda ya uwekezaji katika timu yao, na sasa Yanga imekuwa timu ya ushindani.
Aidha, Ulimwengu amesema anatamani katika droo ya CAF wapangwe na Yanga na atafurahi kucheza dhidi ya timu ya nyumbani.
“Itakuwa mechi nzuri sana sisi na Yanga, yaani mimi nacheza pale Taifa dhidi ya Yanga, tamu sana”.
Mbali na Yanga na Mazembe, timu nyingine zilizofuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ni FUS Rabat, Kawkab Marrakech zote za Morocco, Etoil du Sahel ya Tunisia, Ahli Tripoli ya Libya, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.