Jumamosi , 17th Mei , 2014

Timu ya taifa ya tennis ya walemavu ya Tanzania Wheel Chair Tennis imesema pamoja na kuwa katika hali ngumu kifedha, wachezaji wameweka uzalendo mbele na kusahau shida ili kurejea na medali.

Timu ya taifa ya tennis ya walemavu ya Tanzania Wheel Chair Tennis iko katika maandalizi mazito yakujiandaa na michuano ya kimataifa ya tennis itakayofanyika nchini Kenya na baadae ile ya Africa itakayofanyika nchini Afrika kusini.

Kocha mkuu wa kikosi hicho Riziki Salum amesema pamoja na maandalizi hayo timu hiyo inakabiliwa na ukata wa fedha za nauli za usafiri wa ndani kwa wachezaji hao, maji na kubwa ni fedha za tiketi za kwenda kushiriki michuano hiyo wakianzia na michuano ya Kenya Open ambayo wao ndiyo mabingwa watetezi.

Aidha Riziki amewaomba wadau wa michezo kote nchini kuisaidia timu hiyo kwani haita waangusha kwakuwa imekua ikifanya vema katika michuano mbalimbali ya kimataifa pamoja na kuwa katika hali ya ukata wa fedha.