Jumanne , 5th Apr , 2016

Suala la ukosefu wa pesa ndiyo imekuwa ugonjwa mkuu kwa michezo kwa ngazi ya vilabu na Taifa kuanzia kwa vilabu hadi kwa vyama vya michezo nchini kitu ambacho kimekuwa ndiyo ugonjwa mkuu ambao umekuwa ukiathili maandalizi ya timu kwa ujumla.

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya riadha chini ya miaka 20 ya Tanzania.

Kukosekana kwa pesa kumefanya maandalizi ya timu ya taifa yavijana ya mchezo wa riadha ya umri wa miaka chini ya 20 kuchelewa kuanza kambi rasmi ya maandalizi ya michuano ya ubingwa kwa nchini za Afrika Mashariki na Kati itakayofanyika kuanzia mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Kaimu katibu mkuu wa Riadha Tanzania RT Omben Zavara amesema hali ya ukosefu kwa vyama vya michezo imewakumba na wao mara baada ya kushindwa kuiingiza timu ya vijana iliyoteuliwa hivi karibuni kutoka kwatika michuano ya mashule ya UMITASHUMTA na UMISETA ambayo ilikuwa ianze kambi rasmi April Mosi na sasa itaanza kambi April 14 mwaka huu wiki mbili kabla ya michuano hiyo ya EAC haijaanza kitu ambacho kitaathili maandalizi ya timu hiyo kwakiasi kikubwa.

Ombeni Zavara amesema hayo wakati akithibitisha kubaki kama ilivyopangwa kwa ratiba ya michuano hiyo ya vijana ambayo itafanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuanzia April 29 mwaka huu.

Zavara amesema kumekuwa na minongo'ono ya hapa na pale kuhusu ratiba ya michuano hiyo lakini wao kama wenyeji wanathibitisha kuwa ratiba ya mashindano ya mbio za vijana chini ya miaka 20 ya kuwania ubingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na kati iko pale pale na kimsingi mbio hizo ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji zitafanyika jijini Dar es Salaam ikishirikisha nchini 11 ambazo zimethibitisha.

Aidha Zavara amesema ratiba hiyo iko kama awali mashindano kuanza April 29 mwaka huu na wao kama wenyeji wanaendelea kukamilisha maandalizi yote japo wanakabiliwa na ukata jambo ambalo limefanya hata kambi ya timu ya taifa kusogezwa mbele kutoka April mosi hadi 14.