Ufafanuzi wa TFF kuhusu agizo kwa makocha

Ijumaa , 11th Sep , 2020

Shirikisho la mpira wa miguu ya nchini Tanzania TFF, limetolea ufafanuzi juu ya agizo la Vilabu vyote kuwasilisha wasifu wa makocha wake kwa mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF ,Oscar Milambo akifafanua jambo .

TFF Ilitoa agizo hilo jana kuwa Vilabu viwasilishe vyeti na wasifu wa makocha wao kwa mkurugenzi wa ufundi,Oscar Milambo na mwisho ni setmeba 15 mwaka huu.

Alipoulizwa kwa nini agizo hilo limetolewa wakati ligi imeshaanza ,Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Oscar Milambo amesema inawezekana tamko hilo lakini ni suala la msingi ni kutaa kuhakikisha makocha wanakidhi vigezo vilivyowekwa.

Milambo amesisitiza kwamba vipo vilabu ambavyo bado havijawasilisha wasifu ingawa ni utaratibu ambao upo kila msimu.