Jumatano , 28th Sep , 2022

Mabingwa mara mbili wa kombe la Dunia timu ya taifa ya Argentina imeendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri, wamefikisha idadi ya michezo 35 waliyocheza bila kufungwa hii ni mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Jamaica kwenye mchezo wa kirafiki.

Argentina wamecheza michezo 35 mfululizo bila kufungwa, mara ya mwisho kupoteza mchezo ulikuwa Julai 2019.

Ushindi huu dhidi ya Jamaica sasa Argentina inahitaji ushindi kwenye michezo miwili ijayo ili kuifikia rekodi ya timu ya taifa ya Italia ya kucheza michezo mingi bila kupoteza michezo 37. Mabao ya ushindi ya Argentina kwenye mchezo huo yamefungwa na Julian Alvarez na Lionel Messi aliyefunga mara 2.

Mara ya mwisho Argentina kupoteza mchezo ilikuwa Julai 2, 2019. walifungwa na Brazili mabao 2-0, toka hapo wamecheza michezo 35 bila kupoteza wameshinda michezo 24 sare michezo 11 wamefunga mabao 70 wamefungwa mabao17.

Mabingwa hao wa Dunia mwaka 1978 na 1989 ni moja ya timu inayopigiwa upatu kutwaa ubingwa wa fainali za kombe la Dunia zinazofanyika nchini Qatar mwaka huu kuanzia November 20 hadi Disemba 18, 2022. Wamepangwa kundi C na mchezo wao wa kwanza watacheza dhidi ya Saudi Arabia November 22.