Alhamisi , 29th Sep , 2022

Bondia wa uzito wa juu wa Uingereza Tyson Fury anayeshikilia mkanda wa WBC anataka dau la zaidi ya Trillion 1 kwa pesa ya Tanzania ili apigane na bondia wa Ukraine Oleksandr Usky anashikilia mikanda 4 ya uzito wa juu.

Bondia Tyson Fury anashikilia mkanda wa uzito wa juu wa WBC

Usky amethibitisha kuwa wapo kwenye mazungumzo na Tyson Fury ya kupanga pambano litakalo wakutanisha wababe hao ngumi lakini akaweka wazi kuwa pambano hilo linaweza lisifanyike kutokana na dau analotaka Fury. Bondia hiyo mwingereza anataka dau la Pauni milioni 500 zaidi ya Trillion 1, bilioni 268 na milioni 473 kwa pesa ya Tanzania.

Usky anashikilia mikanda ya WBA Super, WBO, IBO na IBO ameweka wazi kuwa hana mpango wa kupigana ndani ya mwaka huu 2022 na pambano hilo kati yake na Tyson Fury kama wakifikia makubaliano litafanyika mwakani 2023.