Ijumaa , 15th Dec , 2023

Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara ( TPLB) imetupilia mbali shauri la klabu ya Yanga la kutaka marejeo ya adhabu ya kiungo wake Khalid Aucho ambaye amefungiwa michezo 3 na faini ya shilingi laki tano (500,000).

Kiungo wa Yanga SC Khalid Aucho amefungiwa michezo 3 na faini ya shilingi milioni 1 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu.

Taarifa ya TPLB imesema baada ya kupitia meelekezo ya Yanga na kanuni za Ligi, kamati imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia, huku ikimtaka mchezaji huyo kuzingatia mchezo wa kiungwana wakati wote.

Khalid Aucho alifungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya Shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kumpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu kwenye mchezo uliochezwa Novemba 08,2023 Jijini Tanga.