Alhamisi , 12th Jan , 2017

Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania TPBC imetangaza inataraji kuandaa mapambano saba ya ngumi za kulipwa ya kuwania ubingwa kwa mabondia wa hapa nchini yatakayofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwezi ujao.

Mohamed Matumla kushoto katika moja ya mapambano yake.

Rais wa TPBC Chaurembo Palasa ameiambia Hotmix Michezo wameamua kuanza mwaka kwa kuweka mapambano mengi ili kukuza ngumi za kulipwa hapa nchini hasa kwa vijana na kimsingi maandalizi yote yamekamilika.

Hotmix michezo imefanikiwa kuzungumza na mabondia Mohamed Matumla Snake Jr na Mfaume Mfaume watakaopambana Februari 5 mwaka huu ikiwa ni moja kati ya mapambano hayo ambapo kila mmoja ametamba kumkalisha mwenzake siku hiyo.