Jumatatu , 10th Jan , 2022

Nyota wa Golden State Warriors amerejea Uwanjani baada ya miezi 31 aliyokuwa nje akiuugza majeruhi na aliisaidia timu yake kushinda kwa alama 92-82 dhidi ya Cleveland Cavaliers.

Katika mchezo huo Thompson alifunga alama 17 ndani ya dakika 20 baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku 941 tangu apate majeraha kwenye mchezo wa kupoteza katika fainali ya mkondo wa sita dhidi ya Toronto Raptors mwaka 2019.

Thompson mwenye umri wa miaka 31 baada ya kurejea alisema kuwa: “'Nilipata hisia nyingi za zamani ambazo zilinikumbusha mara yangu ya mwisho kuwa uwanjani, leo ilikuwa siku kubwa sana kwangu,”'alisema

Bingwa huyo mara tatu wa NBA akiwa na Golden States Warriors, mwaka 2015, 2017 na 2018 huku akipoteza fainali ya mwaka 2016 na 2019.