Jumapili , 18th Oct , 2020

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limevitaka vilabu kufuata miongozo, kanuni na taratibu endapo vinakuwa havijaridhika na maamuzi ya kesi wanazowasilisha kwenye kamati mbalimbali za maamuzi ndani ya TFF. Wametakiwa kukata rufaa ngazi za juu za TFF, FIFA au CAS.

Makao makuu ya TFF

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Oktoba 18, 2020, TFF imeeleza kusikitishwa na taarifa za upotoshaji juu ya maamuzi ya kesi mbalimbali zinazowasilishwa.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa TFF ni taasisi sio mtu na inaongozwa kwa katiba yake na kanuni mbalimbali hivyo kesi zote zinazowasilishwa zinashughulikiwa kwa muongozo na kwamba Shirikisho hilo halina mamlaka ya kuzuia kesi kwenda kwenye mamlaka za haki.

Soma taarifa kamili hapo chini