Jumapili , 28th Jun , 2015

Pamoja na kufanya vema katika michuano mbalimbali ya kimataifa timu ya taifa ya mchezo wa tenisi ya walemavu ya Tanzania [wheel chair tennis]imekua haina sapoti ya kutosha kwa wadau wa michezo hapa nchini na serikali kwa ujumla hasa katika maandalizi

Baadhi ya wachezaji wa tenisi kwa walemavu [wheel chair tennis] wakichuana jijini Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya tenisi ya walemavu [wheel chair tenis] Riziki Salum amesema mashindano ya kimataifa ya wazi ya tenisi ya Tanzania ambayo yamemalizika jana yamesaidia kuwaongezea uzoefu wachezaji wa kikosi hicho ambacho kinaundwa na chipukizi wengi.

Riziki amesema pamoja na maandalizi wanayofanya kujiandaa na michano ya kimataifa kikosi hicho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi hasa ukosefu wa vifaa na posho za nauli kwa wachezaji wa timu hiyo.

Riziki ameongeza kusema kuwa watu wengi wamekuwa hawaipi nafasi ama kipaumbele timu hiyo ambayo kimsingi pengine ndiyo timu pekee katika timu za michezo mbalimbali hapa nchini ambayo inarekodi bora zaidi katika michuano ya kimataifa.

Amesema timu ya Tanzania ndiyo timu bora namba moja kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati huku ikishika nafasi ya tatu kwa Afrika ikiongozwa na nchi za Afrika kusini na Algeria.